Nidhamu ya kiroho hutufanya tuwe wakamilifu katika roho. Imeandikwa, 1Timotheo 4:7-8 "Bali hadithi za kizee zisizokuwa na dini uzikatae nawe nawe ujizoeze kupata utauwa kwa mnaan akujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo lakini utauwa hufaa kwa mambo yote yani unayo ahadi ya uzima wa sasa na ya ule utakayokuwapo baadaye."
Nidhamu ya kiroho yatufanya tuweje? ya tuwezesha kukimbia na kufaulu katika maisha haya. Imeandikwa, 1Wakorintho 9:24 "Je hamjui yakuwa wale washindanao kwa kupinga mbio hupiga mbio wote lakini apokeaye tuzo ni mmoja pigeni mbio namna hiyo ili mpate."
Nidhamu ya kiroho hutoa mambo yasiyo na maana katika maisha yetu. Imeandikwa, Waebrania 12:1 "Basi nasi pia kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii na tuweke kando kila mzingo mzito na dhambi ile ituzingayo kwa upesi na tupinge mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu."