Mungu amewaahidi wao wanao mwamini Yesu kuwa mwana wa Mungu uzima wa milele. Imeandikwa, Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanwe pekee ili kila mtu amwaniye asipoytee bali awe na uzima wa milele.." Uzima wa milele ni zawadi kwa wale wanao mwamini Yesu. Imeandikwa. 1yohana 5:11-12 "Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu uko katika mwanawe yeye aliye naye mwana anao huo uzima, asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima.
Maisha yetu ya mbiguni yanaanza wakati Yesu anaporudi mara ya pili. Imeandikwa, 1Wathesalonike 4:16-17 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza kasha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."
Wakati Yesu atakaporudi tutafanywa haswa na tufanane naye. Imeandikwa, Kwa maana sisi wennyeji wetu uko mbinguni kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote view chini yake."
Je! Bibili a yasemaje kuhusu mbinguni? Imeandikwa, Yohana 14:2-3 "Nyubani mwa Baba yangu mna makao mengi kama sivyoningaliwaambia maana naenda kuwaandalia mahali basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi mwepo."
Maisha yajayo ya milele ni zaidi ya mafikara yetu. Imeandikwa, 1Wakorintho 2:9 "Lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao."
Isaya alisema nini kuhusu maisha yajayo? Imeandikwa, Isaya 65:21-23 "Nao watajenga nyumba na kukaa ndani yake watapanda mizabibu na kula atunda yake hawatajenga akakaa mtu mwingine ndani yake hawatapanda akala mtu mwingine maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi hawata jitaabisha kwa kazi bure wala hawatazaa kwa taabu kwa sababu wao ni wazao wahao waliobarikiwa na Bwana na watoto wao pamoja."
Amani itakuwapo hata katika jamii ya wanyama. Imeandikwa, Isaya 65:25 "Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na samba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawata dhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote asema Bwana."
Viwete wataponywa. Imeandikwa, Isaya 35:5-6 "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu na ulimi wake aliye bubu utaimba maana katika nyika maji yatabubujika na vijito jangwani."
Mungu ataishi na watu wake, haop ndipo mwisho wa kifo, kilio na maumivu. Imeandikwa, Ufunuo 21:3-4 "Nika sikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu naye atafanya maskani yake pamoja nao nao watakuwa watu wake naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao naye atafutakila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena wala maombolezo wala kilio wala maumivi hayatakuwapo tena kwa kuwa mambo yakwanza yaekwisha kupita."