Tunapaswa kumuabudu Mungu Imeandikwa Zaburi 100:4-5 "Ingieni mlangoni mwake kwa kushukuru; nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake; kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; na uwaminifu wake vizazi na vizazi."
Nenda kanisani ukamtafute Bwana na kufikiri juu yake Yesu. Imeandikwa katika Zaburi 27:4 "Neno moja nimelitaka kwa Bwana, nalo ndilo nitakalolitafuta, nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu niutazame uzuri wa Bwana na kutafakari hekaluni mwake."
Hususan wakati huu wa mwisho ni muhimu zaidi kwenda kanisani. Imeandikwa Waebrania 10:25 "wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."
Mungu ametuahidi kuwa nasi hata katika vikundi vidogo. Imeandikwa katika Mathayo 18:20 "Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu mimi nipo papo hapo katikati yao."
Shukuru kwa kuweza kuabudu kwa uhuru. Imeandikwa katika Zaburi 122:1 "Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani mwa Bwana."
Kwenda kanisani ni kusikiliza na kujifunza. Imeandikwa katika Mhubiri 5:1 "Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; maana ni heri kukaribia ili usikae, kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; ambao hawajui kuwa wafanya mabaya."
Twaenda kanisani kupatana na Mungu. Imeandikwa katika Habakuki 2:20 "Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake."
Yesu alitupa mfano wa kwenda kanisani. Imeandikwa katika Luka 4:16 "Akaenda Nazareti hapo alipolelewa na siku ya Sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyo desturi yake, akasimama ili asome."