Je ndoa yatakiwa kudumu muda gani? Imeandikwa Warumi 7:2 "Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapo kuwa yu hai bali akifa yule mume amefunguliwa ile sheria ya mume."
Mungu amkubali kuivunja ndoa katika kanuni moja tuu!. imeandikwa Mathayo 5:32 "Lakini mimi nawaambia, kila mtu amuachaye mkewe isipokuwa kwa habari ya uasherati amefanya kuwa mzinzi na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini."
Mungu anachukizwa nao wanao vunja ndoa kwa wale ambao wemekuwa waaminifu kwao. Imeandikwa Malaki2:14-16 "Lakini ninyi wasema Nikwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako uliyemtendae mambo ya hiana angawa yeye ni mwenzako na mke wa agano lako. Hakuna mtu moja aliyetenda hivi ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha mungu? kwahiyo jihadharini roho zenu mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi na kuchukia kuachana asema Bwana, Munugu wa Israeli naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu na mchukia, asema Bwana wa majeshi, basi jihadhari roho zenu msije mkatenda kwa hiana."
Mtu akihiana sharti akae bila mke au bila kuoa imeandikwa 1Wakorintho 7:10-11 "Lakini wale walio kwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi ila Bwana; mke asiachane na mumewe lakini akiwa ameachana naye na akae asiolewe, au apatane na mumewe tana mume asimache mkewe."
Kuowa mtu asiye amini si msingi wakuvunja ndoa. Imeandikwa 1Wakorintho 7:12-14 "Lakini wengine nawaambia mimi wala si Bwana ya kwamba iwapo ndugu mmoja na mke asiyeamini, na mke huyo ankubali kukaa naye asimwashe mumewe kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mke na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe kama isingekuwa hivyo watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu."