Mali niya siku chache tu. Imeadikwa, Walawi 25:23 "Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa kwani nchi ni yangu mimi maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu."
Tusiwashe mali itutawale. Imeandikwa, Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu ama atashikamana na kumdharau huyu hamwezi kumtumikia Mungu na mali." hamwezi kumtumikia Mungu na mali." Luka 12:15 Akawaambia aganlieni jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa mali yake aliyo nayo."
Mali haileti furaha. Imeandikwa, Wafilipi 4:12-13 "Najua kudhiliwa tena najua kufanikiwa, katika hali yo yote na katika mambo yo yote nimefundishwa, kushiba na kuona njaa na kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayeweza ambo yo yote katika yeye anitiaye nguvu."
Haifai kusumbukia mali bali nyumba ya Mungu. Imeandikwa, Hagai 1:9 "Mlitazamia vingi kumbe vikatoka vichache tena mlipo vileta nyumbani nikavipeperusha ni kwa sababu gani? asema Bwana wa majeshi Ni kwasababu ya nyumba yangu invyokaa hali ya kuharibika wakati ambapo ninyi mnakibilia kila mtu nyumbani kwake."
Tu wasadie wenye mahitaji. Imeandikwa, Matendo ya mitume 2:44-46 "Na wote waliyoamini walikuwa pamoja na kuwana vitu vyote shirika wakiuza mali zao na vitu vyao walivyokuwa navyo na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haya. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu wakimega mkate nyumba kwa nyuba na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe."