Mungu anataka roho iliyokamili bali si kafara. Imeandikwa Zaburi 50:13-15 "Je nile nyama ya mafahali au ninywe damu ya mbuzi mtolee Mungu dhabihu za kushukuru mtimizie aliye juu nadhiri zako ukanite siku ya mateso nitakuokoa nawe utanitukuza."
Ungu anapendezwa na kujitole kwetu na mali yetu kwake. Imeandikwa, Mathayo19:21 "Yesu akamwambia ukitaka kuwa mkamilifu enenda ukauze ulivyo navyo uwape maskini nawe utakuwa na hazina mbinguni kish anjoo unifuate."
Mungu hufurahiswa na maisha ya kujitolea kwani ni heshima kw neema yake. Ieandikwa, Warumi 12:1 "Basi ndugu zangu na wasihi kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kupendeza Mungu ndiyo ibada yenu yenye maana."
Mungu hufurahiswi na huduma zetu zinazo toka katika moyoni wetu, hujichukua kama kafara. Imeandikwa, Waebrania 13:15-16 "Basi kwa njia yake yeye na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima yani tunda la midomo iliungamayo jina lake."