Viumbe vya asili vyaonyesha jinsi Mungu alivyo. Imeandikwa, Zaburi 19:1 "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu Na anga laitangaza kazi ya mikono yake."
Nguvu za Mungu za tawala maumbile. Imeandikwa, Mathayo 8:26 "Akawaambia mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? mara akaondoka akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamaka wakisema huyu nimtu wanamna ghani hata pepo za bahari zamtii?."
Maumbile yaonyesha kuwa Mungu yupo. Imeandikwa, Warumi 1:20 " Kwasabubu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana na kufahamika kwa kazi yake yani uweza wake wa milele na uungu wake hata wasiwe na udhuru."
Maumbile yanangojea kukombolewa kutaka kwa uharibifu wa dhambi. Imeandikwa, Warumi 8:19-20 "Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu kwa maana viumbe vyote vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yakeila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewe katika utumwa wa uharibifu hataviingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu."