Home / Masomo ya Biblia / Vijana/Watoto

Vijana/Watoto

Ujana ni wakati mwema wa kutengeneza uhusiano na Mungu. Imeandikwa, Mhubiri 12:1 "Mkumbuke Muuba wako katika siku za ujana wakokabla hazijaja siku zilizo mbaya wala haijakaribia miaka utakaposema mimi sina furaha katika hiyo."

Mungu anahitaji kujitolea kuliko ujana. Imeandikwa, 1Samueli 2:18 "Lakini Samueli alikuwa akitumika mbele za Bwana naya alikuwa kijana mwenye kuvaa naivera ya kitani."

Mungu anatazamia nini kutoka kwa watoto? Imeandikwa, Wakolosai 3:20 "Nanyi watoto watiini wazazi wenu katika mambo yote; Maana jambo hili la pendeza katika Bwana."

Amri ya Mungu yasemaje kuhusu watoto? Imeandikwa, 20:12 "Waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipata kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako."

Watoto wapaswa kuwatii wazazi wao kwa muda kiasi gani?. Imeandikwa, Mithali 23:22 "Msikilize baba yako aliyekuzaa wala usimdharau mama yako aliyekuzaa."

Kuwa na nidhamu yaonnyesha upendo wa wazazi. Imeandikwa, Mithali 13:24 "Yeye asiye tumia fimbo yake humchukia mwanawe bali yeye ampendaye humrudi mapema."

Vijana wawezakuwa na mfano kama wa Kristo. Imeandikwa, 1Timotheo 4:12 "Mtu awaye yote asiudharau ujana wako bali uwekielelezo kwao waaminio katika usemi na mwenendo na katika upendo, na imani na usafi."

Watoto wapaswa kuelimika kutokana wazazi wao. Imeandikwa, Mithali 1:8 "Mwangu yasikilize mafundisho ya baba yako, wala usiiache sheria ya mama yako."

Kuishi maish ya mabaya nikuto heshimu wazazi. Imeandikwa, Mithali 28:7 "Yeye aishikeye sheria ni mwana mwenye hekima bali yeye aliye rafiki wa walafi humuaibisha babaye."

Nivibaya kuwa tumia wazazi wako kwa njia isiyo njema. Imeandikwa, Mithali 28:24 "Aibaye mali ya babaye au mamaye na kusema si kosa mwana huyo ni rafiki wa mtu haribifu."

Vijana wapaswa kuwachagua vema rafiki zao. Imeandikwa, 2Timotheo 2:22 "Lakini zikimbie tama za ujanani, ukafuate haki na imani na upendo pamoja na wale wamwitao Bwana kw moyo safi."