Wakristo hawapwaswi kujihusisha na miujiza ya uganga. Imeandikwa, Matendo ya mitume 19:18-19 "Na wengi walio amini wakaja wakaungama wakithihirisha matendo yao na watu wengi waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao wakavichoma vitabu mbele ya watu wote wakafanya hesabu ya dhamani yake wakaona yapata fedha hamsini helfu."
Ufanyaji wa uganga ni chukizo machoni pa Mungu. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 18:9-13. "Utakapo kwisha ingia katika nchi akupayo Bwana Mungu wako usijifunze kutenda mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane mtu apitishaye mwanaye au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye bao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi au mtu awaombeaye wafu kwa maana mtu atenaye hayo ni chukizo kwa Bwana kasha ni kwasababu ya hayo Bwana, Mungu wako anawafukuza mbele yako uwemkamilifu kwa Bwana Mungu wako."