Ngoa

Tamaa ni mojawapo ya vitu vya ulimwengu. Imeandikwa, 1Yohana 2:16-17 "Maana kila kilicho duniani, yaani tamaa ya mwili na tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu atadumu hata milele."

Tamaa ya mwili ni dhambi. imeandikwa, Mathayo 5:28 "Lakini mimi na mwambia kila atazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Mtu mwenye tamaa atalipa mavuno yake. Imeandikwa, Mithali 6:25-29. "Usiutamani uzuri wake moyoni mwako wala usikubali akunase na kobe zake za macho yake maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya dhamani je? mtu aweza kuua moto kifuani pake, na nguo zake zisiteketezwe? je? mtu aweza kukanyaga makaa ya moto na nyayo zake zisiungue? ndiyo ilivyo mtu aingiaye kwa mke wa jirani yake kila mtu amguzaye huyo atakuwa na hatia."

Neema ya Mungu ya tusaidia kuikataa tamaa. Imeandikwa, Titu 2:11-12 "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo ya tufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kishi kwa kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa."