Wakati wa kiama watu wa Mungu watakwenda mbinguni. Imeandikwa, 1 Wathesalonike 4:16-17 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malika mkuu na parapanda ya Mungu nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza; kisha sisi tulio hai tulio salia tutanyakuliwa pamoja Bwana milele."
Wakati Yesu atakapokuja wenye dhambi watajawa na hofu na mushtuko mkuu. Imeandikwa, Ufunuo 6:16-17 "Watakimbia wakiiambia milima na miamba tuangukieni tusitirini mbele za uso wake yeye aketiye mbele cha kiti cha enzi na hasira ya mwana kondoo kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao imekuja naye ni nani awezaye kusimama?."
Viongozi wa wenye dhambi watamalizwa na mwanga wake nao wenye dhambi watauwawa kwa upanga wake. Imeandikwa, 2Wathesalonike 2:8 "Hapo ndipo atakapofuniliwa yule asi ambay e Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake." Ufuno 19:21 yasema "Na wale walio salia waliuawa kwa upanga wake yule aliye keti juu ya yule farasi upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao."
Kwa kuwa watakatifu waekwenda kuwa na Yesu mbinguni, wenye dhambi watauawa kwa miali yeke Yesu, nayo dunia itakaa bila kitu kilicho na uhai kwa mada. Imeandikwa, Yeremia 4:23-25 "Naliangalia nchi na tazama ilikuw aukiwa; haina watu na liangalia mbingu nazo zilikuwa hazina nuru naliangalia milima natazama ilitetemeka na milima yote ilisongea huko na huko naliangalia na tazama hapakuwana mtu hata mmoja na ndege wote wa angani amekwenda zao."
Wenye dhambi watakuwa kwenye kaburi kwa miaka elfu moja. Imeandikwa, Ufunuo 20:4-5 "Kisha nikaona viti vya enzi wakaketi juu yake nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao wao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na kwa ajili ya neno la mungu no wasiomsujudia yule mnyama wala sanamu yake wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao wala katika mikono yao nao wakawa hai wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu hao wafu walio salia hakuwa hai hata itimie ile miaka elfu."
Wakiwa mbinguni na Yesu hao watakatifu, na wenye dhambi wamekufa shetani atakuwa gerezani miaka elfu. Imeandikwa, Ufunuo 20:1-3 "Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni mwenye ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwamkononi mwake akamshika jule joka yule nyoka wa zamani ambaye ni Ibilisi na Shetani akamfunga miaka elfu akatupa katika kuzimu akamfunga akamtua mhuri juu yake asipate kuwadanganya mataifa tena hata ile iaka elfu itimie na baada ya hayo yapasa afunguliwe mda mchache."
Baadaya miaka elfu moja mji mtakatifu utashuka kutoka mbinguni an kuja hapa duniani. Imeandikwa, Ufunuo 21:1-3 "Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya kwa maana nchi za kwanza na mbingu za kwanza zimekwisha kupita wala hapana bahari tena nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu umewekwa tayari kama bi-biarusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi, ikisema tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu naye atafanya maskani yake pamoja naye nao watakuwa watu wake naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao."
Baada yake shetani kufunguliwa na wenye dhambi kufufuliwa, watajaribu kuunyakuwa uleji mtakatifu wa Mungu. Imeandikwa, Ufunuo 20:7-9 "Na hiyo mika elfu itakapokwisha shetani atafunguliwa atioke kifungoni mwake naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na magogu kuwa kusanya kwa vita ambayo hesabu yao nikama shanga wa bahari wakapanda juu ya upanawa nchi wakaizingira kambi ya watakatifu na mji huo uliopendwa moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala."