Je! baraka ya vitu ya toka wapi? Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 8:18 "Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri. ili alifanyaye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo."
Je twaweza kuweka fedha mbelya ya Mungu au ya vitu vilivyo bora?. Imeandikwa, Yeremia 9:23-24 "Bwana asema hivi mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake wala tajiri asijisifu kwa utajiri wake bali ajisifuye ajisifu kwa sababu hii ya kwamba amenifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana nitendaye wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asema Bwana.."
Utajiri wawezas kutupa mafikara mabaya kuhusu vitu. Imeandikwa, Luka 12:15 "Akawaambia angaliyeni jilindeni na choyo maana uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."
Sivema kufanya mali kuwa nia yako kumbwa.
Imeandikwa, Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili kwamaana atamchukia huyu na kumpenda huyu ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu hamwezi kumtumikia Mungu na mali." 1Timotheo 6:9 yasema "Lakini hao watakao kuwa na mali huwanguka katika majaribu na tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu."
Nivigumu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Imeandikwa, Marko 10:23-25 "Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake jinsi itakavyo kuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake Yesu akajibu tena akawaambia watoto jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu ni rahisi ngamia kupenya katika shimo la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
Tamaa ya pesa ni dhambi Imeandikwa, 1Timotheo 6:10 "Maana shina moja la mabaya ya kila namna nikupenda fedha ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi."
Tamaa huleta vita. Imeandikwa, Yakobo 4:1-2 "Vita vyatoka wapi na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? si humu katia tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu mwatamani wala hamna kitu mwauwa na kuona wivu wala hamwezi kupata mwafanya vita na kupigana wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi."
Ni kweli unapotoa kwa wingi ndivyo utakavyo lipwa au barikiwa. Imeandikwa, Luka 12:33-34 "Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka jifanyieni mifuko isiyochakaa akiba isiyopungua katika mbingu mahali pasipokaribia mwivi wala nondo haharibu kwa kuwa hazina yenu ilipo ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu."
Mungu anataka tutumie vipi fedha zetu? Imeandikwa 1Timotheo 6:17-19 "Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune wala wasiutumainie utajiri usio yakini bali wamtumaini Mungu atupye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha watende mema wawe matajiri, kwa kutenda mema wawe tayari kutoa mali zao washirikiane na wengine kwa moyo huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao ili wapate uzima ulie kweli kweli."
Ninani mwenye mali yetu?. Imeandikwa, Mambo ya walawi 25:23 "Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa kwani nchi ni yangu mimi maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu."
Kutosheka hakuletwi na wingi wa mali au fedha ulizo nazo. Imeandikwa, Wafilipi 4:12-13 "Najua kudhiliwa na tena kufanikiwa katika hali yo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa kuwa na vingi na kupungukiwa nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."
Mungu ametuagiza tumrudishie zaka na sadaka naye atatubariki. Imeandikwa, Malaki 3:8-10 "je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini niyni mnaniibia mimi lakini ninyi mwasema tumekuibia kwa namna gani? mmenibia kwa zaka na dhabihu ninyi mmelaniwa kwa laana maana mnaniibia mimi naam taifa hili lote leteni zaka kamili ghalani ili kiwepo chakula katika nyumba yangu. Mkanijaribu kwa njia hiyo asema Bwana wamajeshi mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha au la."
Imeandikwa, Mathayo 23:23 "Ole wenu waandishina mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari za jira lakini mmeacha mambo makuuya sheria yani adilina rehema na imani hayo imewapasa kuyafanya wala yale mengine msiyaache."