Home / Masomo ya Biblia / Matukano

Matukano

Maongezi yetu yanapaswa kuwa vipi? Imeandikwa katika Waefeso 5:4 "Wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo haya pendezi; bali afadhali kushukuru."

Amri moja yatuonya kutotumia jina la Mungu bure. Imeandikwa katika Kutoka 20:7 "Usilitaje jina la Bwana Mungu wako bure, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure."

Mungu ametuonya kutotumia lugha chafu. Imeandikwa katika Wakolosai 3:8 "Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na matusi vinywani mwenu."
Katika maongezi twaweza kutofautisha mtu. Imeandikwa katika Mithali 13:3 "Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake. Bali afunuaye midomo yake, atapata uharibifu."

Wafuasi wa Yesu wapaswa kuongea kwa uzuri na katika hali ya uangalifu. Imeandikwa katika Wakolosai 4:6 "Maneno yenu yawe na neema siku zote yakikolea munyu mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu."

Maongezi yetu yaweza kuwa na mvuto kwa watu wengine. Imeandikwa katika 1Timotheo 4:12 "Mtu awaye yote asiudharau ujana wako bali uwe kielelezo kwa wao waaminio katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi."