Mungu jutumia watu kujibu mahitaji yao. 2Wafalme 6:6-7 "Mtu wa Mungu akasema, kilianguka wapi? akamwonyesha mahali akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea akasema kiokote basi akanyosha mkono wake akakiokota."
Ni vema kujitole kuwasaidia watu. Imeandikwa, Mathayo 23:11-12 "Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtuwa wenu. Na ye yote atakayejikweza atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa."
Kufahamu yakuwa unapo wasaidia watu unamtumikia Mungu. Imeandikwa, Mathayo 25:40 "Na mafalme akajibu akawaambia amni nawaambia kadiri ya jinsi malivyomtendea mmojwapo wa hao ndungu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi."
Mungu awezakua ametupa vitu tulivyonavyo kujibu mahitaji yetu. Imeandikwa, Ruthu 2:2-3 "Naye Ruthu Mmoabi akawabia Naomi sasa naenda kondeni niokote masaso ya masuke nyuma yake yule yule ambaye nitaona kibali machoni pake akamwambia haya mwanagu nenda. Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji na bahati yake ikamtukia kwaba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi ambaye alikuwa wa jamaa ya Elimeleki."
Tumtegemee Mungu katika kila jambo na kumpa mahitaji yetu. Imeandikwa, Zaburi 104:27-28 "Hao wote wanakungoja wewe uwape chakula chao kwa wakati wake wewe huwapa wao wanakiokota wewe waukunja mkono wako wao wanashiba mema."
Mahitaji yetu ya kila siku ya mwili ni ya maana kwake Yesu. Imeandikwa, Marko 8:1-3 "Katika siku zile, kwavile ulivyo kuwa mkuu tena ule mkutano nao wamekosa kitu chakula akawaita wanafunzi wake akawaambia, nawahurumia makutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami wala hawana kitu cha kula nami nikiwaanga waendezao nyumbani kwao hali wanafunga watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali..."