Home / Masomo ya Biblia / Machafuko

Machafuko

Unapochanganyikiwa, omba uongozi wa Mungu. Imeandikwa katika Mithali 2:1-8 "Mwanangu kama ukiyakubali maneno yangu, na kuyaweka akiba maagizo yangu hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukaulegeza moyo wako upate fahamu; naam ukiita busara, na kupaza sauti yako upate ufahamu; ukitafuta kama fedha na kuutafutia kama hazina iliyositirika; ndipo utakapofahamu kumcha BWANA nakupata kumjua Mungu, kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu apate kuyalinda mapito ya hukumu, na kuhifadhi njia ya watakatifu wake."

Bila shauku uliza Mungu ufahamu. Imeandikwa katika Yakobo 1:5-8 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima naaombe dua kwa Mungu awapaye wote kwa ukarimu wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani pasipo shaka yo yote maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku maana mtu kama yule asidhani yakuwa atapokea kitu kwa BWANA mtu wania mbili asita-sita katika njia zake zote."

Ukiwa umechanganyikiwa juu ya maisha yako ya kesho muulize Mungu kwa msaada imeandikwa katika Zaburi 32:8-9 "Nitakukufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri jicho langu likikutazama. Msiwe kama farasi wala nyumbu walio hawana akili. Kwa kwa matandiko ya lijamu na hatamu sharti kuwa zuia hao, au hawatakukaribia."

Usijiamini wakati umechanganyikiwa. Imeandikwa katika Mithali 3:5-8 "Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako yote usiwe mwenye hekima machoni pako; mche BWANA ukajiepusha na uovu. Itakuwa afya mwilini pako na mafuta mifupani mwako."