Twaweza kufarijika kutoka na mifano ya watu wengine imeandikwa 1Wathesalonike 3:7 "Kwa sababu hiyo ndugu tulifarijiwa kwa habari zenu katika msiba wa dhiki yenu yote kwa imani yenu." Maisha ya milele yana tufariji imeandikwa 1Petro 1:6 "Mnafurahi sana wakati huo ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo ikiwa nilazima mmehuzunushwa kwa majaribu ya inambalimbali;"
Tunatiwa moyo kwa kuwapa moyo wengine. Imeandikwa katika Warumi 1:11-12 "Kwa maana ninatamani sana kuwaona nipate kuwapa karama ya rohoni ilimfanywe imara yaani ilitufarijiane mimi na ninyi kila mtu kwa imani ya mwenzake yenu na yangu."
Kufarijiwa kwa mambo ambayo Mungu alitutendea hapo awali imeandikwa Yoshua 24:16-17 "Hao watu wakjibu wakasema hasha! tusimche Bwana ili kuitumikia miungu mingine kwa maana Bwana mungu wetu yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya misri kutoka nchi ya utumwa yeye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya maho yetu nakutulinda katika nia yote ile tuliyoiendea na kati ya watu wa mataifa yote tulio pita katikati yao."
Wakuzeni watu wengine kwa mambo maziri imeandikwa 1Wathesalonike 5:11 "Basi farijianeni kwa kujengana kila mtu na mwenzake vile vile kama mnavyofanya."
Mwafariji washiriki wapia imeandikwa Matendo ya mitume 14:21-22 "Hata walipo kwisha kuihuburi ile injili katika mji ule na kupata wanafunzi wengi wakarejea mpaka listra na ikoni na antiokia, wakiifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile imani na ya kwamba wametupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi."
Wafariji ni viongozi wa makanisa imeandikwa 1Wathesalonike 5:12-13 "Lakini ndungu tunataka mwatambue wale wanaojitambulisha kwa ajili yenu na kwa kuwasimamia ninyi katika Bwana na kuwaonyeni."
Mungu anatufariji tukiwa katika dhiki imeandikwa Yeremia 29:11 "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana nimawazo ya amani wala simawazo ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho."
Mungu atatusaidia wakati tunapo hitaji msaada wa faraja imeandikwa Zaburi 138:3 "Siku ile niliyo kuita uliniitakia ukanifariji nafsi yangu kwa kutnitia nguvu."
Kwa kukufariji bado hatujakamilika naye mungu angali anasaidia imeandikwa Wafilipi 1:6 "Nami niliaminilo ndilo hili ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya kristo yesu."