Jambo la kwanza la kutatua shida nikuwa na mahoji au habari kamili. Imeandikwa, Mithali 18:13 "Yeye ajibuye kabla hajasikia, niupumbavu na aibu kwake."
Jamboa la pili la kutatua shida ni kukubali mawazo papia. Imeandikwa, Mithali 18:15 "Moyo wa mwenye busara hupata maarifa na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa."
Jambo la tatu la kutatua shida nikusikia malalamiko ya walalamishi wote pande zote. Imeandikwa, Mithali 18:17 "Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa anahaki; lakini jirani yake huja na kumchunguza."
Je! Mungu antaka tuzitatue shia vipi? Imeandikwa, Yakobo 1:2-4 "Ndungu zangu hesabuni yakuwa nifuraha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu yakuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi naiwena kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu bila kupungukiwa na neno."
Taabu zaonyesha ya kuwa tunatayarishwa kwa ufalme wa mbinguni. Imeandikwa, 2 Wathesalonike 1:5 "Ndiyo ishara hasa ya kuhukumu iliyo haki ya Mungu ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuingia katika ufale wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa."
Tushukue shida kwa namna gani?. Mungu aweza kutusaidia. Imeandikwa, Zaburi 145:14 "Bwana huwategemeza wote waangukao. Huwainua wote walioinama chini."
Yesu wakatimwingine hutuokoa kutokana na mizigo ya taabu na shida. Mathayo 11:28 "njoni kwangu ninyi yote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."
Amini ya kuwa mpango wa Mungu katika maisha yako ni mwema. Imeandikwa, Warumi 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."
Unashida kutatua shida zako? Mungu atakusaidia. Imeandikwa, Yakobo 1:5 "Lakini mtu wakwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku."
Mwamini Mungu wala si wewe mwenyewe. Imeandikwa, Mithali 3:4-6 "Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri mbele za Mungu na mbele za mwanadamu mtumaini Bwana kwa moyo wako wote walausizitegemee akili zako mwenyewe katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako."