Jina

Majina ya watu katika bibilia yaonyesha tabia ya watu. Imeandikwa, Mwanzo 32:27-28 "Akamuuliza jina lako ni nani? akasema yakobo. Akamwabia, jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli maana umeshindana na Mungu, na watu nawe umeshinda."

Kuheshimu jina la Mungu ni kumuheshimu Mungu. Imeandikwa, Kutoka 3:14-15 "Mungu akamwambia Musa MIMI NIKO AMBAYE NIKO akasema ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO, amenituma kwenu. Tena Mungu akamwambia Musa waambieni wana wa Israeli maneno haya, Bwana Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo amenituma kwenu hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote."

Kutaja jina la Mungu bure huleta adhabu. Imeandikwa, Kutoka 20:7 "Usilitaje jina la Bwana Mungu wako bure maana Bwana hatauhesabia kuwa hana hatia alitajaye jina lake bure."

Jina la Yesu laleta uponyaji na imani. Imeandikwa, Matendo ya mitume 3:16 "Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua na imani ile iliyo kwake yeye amempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote."

Kuna wokovu katika jina lake Yesu. Imeandikwa, Matendo ya mitume 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote kwa maana hakuna jina jingine chni ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."