Jina Yesu nitakatifu toka hapo mwanzo naye akawa wanadanu. Imeandikwa Yohana 1:1, 14 "Hapo mwanzo kulikuwapo neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu, Naye neno alifanyia mwili akaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utkufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli."
Je! kwanini ilimpasa Yesu kuwa mwanadamu? Imeandikwa, Waebrania 2:17 "Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yoteapate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema Mwaminifu katika mambo ya Mungu ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake."
Yesu alionyesha utukufu wake na ubinadamu wake kwa kuyashinda majaribu. Imeandikwa, Waebrania 4:14-15 "Basi iwapo tuna kuhani mkuu aliye ingia katika mbingu, Yesu mwana wa Mungu natuyashike sana maungamo yetu kwa kuwa hana kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yote ya udhaifu bali yeye alijaribiwa sawasawa nasisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi."
Yesu alionyesha utukufu wake kwa kufufuka kwake. Imeandikwa, Mrko 16:6, "Naye akawaambia msistaajabu mnamtafuta Yesu mnazareti aliyemsulubiwa amefufuka hayupo hapa patazameni mahali walipo mweka lakini enendeni zenu kawaambie wanfunzi wake, na perto, yakwamba awatangulia kwenda Galilaya hukomtamwona kama alivyowaambia."
Paulo alionyesha utkufu wa Yesu. Imeandikwa, Wakolosai 2:9 "Maana katika yote unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili."
Uhusiano wa Yesu na Baba yeke niupi? Imeandikwa, Yohana 10:30 "Mimi na Baba tu umoja."
Yesu ndiye tabibu mkuu. Imeandikwa, Luka 8:47-48 "Yule mwanamke alipoona yakwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka akaanguka mbele yake akamweleza mbele za watu wote sababu yake ya kumgusa na jinsi alivyoponywa mara akamwambia binti imani yako imekuponya enenda zako na amani."
Kitambo kidogo kila mtu atakiri kuwa Yesu ni Bwana. Imeandikwa, Wfilipi 2:9-11 "Kwa hio Mungu alimwadhimisha mno akamkirimia jina lile lipitalo kila jina ili kwajina la yesu kila goti lipigwe la vitu vya mbinguni na duniani n akwa chini ya nchi na kila ulimi ukiri yakuwa YESU KRISTO NI BWANA kwa Utukufu wa Mungu Baba."
Yesu anawahiiza watu kutubu dhambi zao. imeandikwa, Mathayo 4:17 "Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia."
Yesu hakuja kuondoa sheria bali kuzikamilisha. Imeandikwa, Mathayo 5:17 "Msidhani yakuwa nilikuja kuitangua tora au manabii la, wala sikuja kutangua bali kutimiliza."
Yesu ndiye njia kwa Mungu. Imeandikwa, Yohana 14:6 "Yesu akamwambia mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi."
Yesu ndiye ufufuo. Imeandikwa Yohana 11:25 "Yesu akamwambia mimi ndimi huo ufufuo, na uzima yeye aniaminiye mimi ajapokufa atakuwa anaishi."
Kazi ya Yesu ilileta utofauti katika maisha ya watu. Imeandikwa, Mathayo 4:23 "Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote akifundisha katika masinagogi yao na kuihubiri habari njema ya ufalme na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu."
Je? mtu afanye nini ili wawe mfuasi wa Yesu? Imeandikwa, Luka 9:23 "Akawaabia wote mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake kila siku."
Maisha yake Yesu yakawa maisha yatu. Imeandikwa Wagalatia 2:20 "Nimesulubiwa pamoja Kristo lakini ni hai bali si mii tena bali Kristo yu hai ndani yangu na uhai nilio nao sasa katika mwili ni nao katika imani ya mwana wa Mungu ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu."
Tujitahidi tuwe kama Yesu. Imeandikwa Wafilipi 2:5 "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya Kristo Yesu."
Twaweza kumjua Yesu kama mwokozi wetu. Imeandikwa Yohana 1:12 na 1Petro 3:18. "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu ndio walewaliaminilo jina lake." "Kwa maana naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki ili atulete kwa Mungu mwili wake akauawa bali roho yake akahuiswa."