Wakati au muda wa Mungu ni haswa. Imeandikwa, Warumi 5:6 "Kwa maana hapo tulipo kuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimiaKristo alikufa kwa ajili ya waovu."
Wakati wa Mungu unatawaliwa na upendo wake. Imeandikwa, 2Petro 3:8-9 "Lakini wapenzi msilisahu neno hili, ya kwamba, kwa Bwana siku moja nikama miaka elfu, na miaka elfi nikama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama wengine wanavyo kudhani kukawia bali huvumilia kwenu maana hapendi mtu ye yote apotee bali wote wafikilie toba."
Kuna wakati wa kilajambo katika ulimwengu. Imeandikwa, Mhubiri 3:1-8 "Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa, wakati wa kuuwa na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga. Wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakti wa kucheza wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe; wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza; wakati wa kuweka na wakati wa kutupa. Wakati wa kurarua na wakati wa kushona; wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena. Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia wakati wa vita na wakati wa amani."