Hakina kitakacho tutennga na Mungu. Imeandikwa, Warumi 8:38-39 "Kwa maana nimekwisha kujua katika ya kwamba wala mauti wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo wala yatakayokuwapo, wala uwezo, wala yaliyo juu wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu uliyoko katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Upendo wa Mungu ni wakujitolea. Imeandikwa, Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele."
Upendo wa Mungu hudumu milele. Imaendikwa, Zaburi 136:1 "Mshukuruni Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele."
Twafafanua upendo nana gani? Imeandikwa, 1Wakorintho13:4-7 "Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hausudu; upendo hautabakari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti ambo yake; hauoni uchungu hauhesabu mabaya haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli huvumilia yote; huamini yote hutumaini yote hustahimili yote; upendo haupungui neno wakati wo wote bali ukiwapo unabii utabatilika zikuwapo lugha zitakoma yakiwapo maarifa yatabatilika kwa maana tuna fahamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu."
Tumeamuriwa kupendana. Imeandikwa, 1Yohana 2:7-8 "Wapenzi siwaandikii amri mpya ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia tena na waandikia amri mpya neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kunga'aa."
Upendo sio kwa marafiki pekee. Imeandikwa, Mathayo 5:43, 44 "Mmesikia kwamba imenenwa upende jirani yako, na, umchukie adui yako, lakini imi nawaambia wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi."
Amri za Mungu zifunkwa kwa neno la upendo. Imeandikwa, Mathayo 22:37-40 "Akamwambia mpende Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni yakwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii."
Twaonyesha upendo wa wetu kwa Mungu katika sheria za Mungu. Imeandikwa, 1Yohana 5:3 "Kwa maana hukundiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake wala amri zake si nzito."
Usifanye upendo wa Mungu udhofike. Imeandikwa, Ufunuo 2:4-5 "Lakini ni neno juu yako ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanzabasi mkumbuka niwapi ulikoanguka ukatubu ukafanye matendo ya kwanza."