Viongozi wema huwapongeza wafanyikazi wao. Imeandikwa, Kutoka 39:43 "Musa akaiona hiyo kazi yote, natazama walikuwa wameimaliza; vile vile kama Bwana alivyoagiza walikuwa wameifanya vivyo; basi Musa akawaombea heri."
Viongozi wema hujua mipaka yao. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 1:9 "Nami wakatiule niwaambia nikasema siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu."
Viongozi kamili huwa watumishi. Imeandikwa, Luka 22 :25 "Akawaambia wafalme wamataifa huwatawala na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili."
Viongozi waonyeshe kuwa wao wana bidii katika kazi zao. Imeandikwa, Mhubiri 9:10 "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri, wala maarifa wala hekima huko kuzimu uendako wewe."
Wahudumie waliochini yako kama vile wewe unavyotaka kuhudumiwa. Imeandikwa, Luka 6:31 "Nakama mnavyotaka watu wawatendee ninyi watendeeni vivyo hivyo."
Kuwa kiongozi sikazi rahisi usife moyo. Imeandikwa, 2Mambo ya nyakati 15:7 "Ninyi jipeni nguvu wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na ijara."
Kiongozi mwema hufuata maangizo ya Mungu. Imeandikwa, Isaya 30:21 "Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema njia ni hii, ifuateni, mgeukapo kwenda mkono wa kushota."
Je! viongozi wa makanisa wapaswa kuwa vipi?. Imeandikwa, 1Timotheo 3:1-7 "Neno la kuaminiwa, mtu akitaka kazi ya askofu atamani kazi njema. basi imepasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja wenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji ajuaye kufundisha. Si mut wa kuzoelea ulevi si mpiga watu, bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu [yani mtu asiyejua kuisimamia nyuba yake mwenyewe atalitunzaje kanisa la Mungu] wala asiye mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi."
Kuna msaada kwa viongozi walio na shida. Imeandikwa, Yakobo 1:5 "Lakini mtu kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa."
Viongozi wema hupanga mambo yao mapema. Imeandikwa, Luka 14:28-30 "Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwaba anavyo vya kuumaliza? asije akashindwa kuumaliza baada ya kupiga msingi, watu wote waonao wakanza kumdhihaki, wakisema mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kuualiza."
Kiongozi mwema hutafuta mawaitha kutoka kwa watu wengine. Imeandikwa, Mithali 15:22 "pasipo mashauri makusudi hubatilika. Bali kwa wingi wa washauri hudhibitika."
Kiongozi mwema huvumilia. Imeandikwa, Mithali 16:32 "Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; na mtu aitwalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji."