Maombi ni hali ya kuongea na Mungu. Imeandikwa, Zaburi 4:3 "Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa Bwana atasikia nimwitapo."
Maombi ni haki. Imeandikwa. Waebrania 4:16 "Basin a tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."
Twaweza kumkaribia Mungu. Imeandikwa, Zaburi 65:2 "Wewe usikiaye kuomba, wote wenye mwili watakujia."
Je Mungu akotayari kusikia maombi yetu na kutujibu? Imeandikwa, Mathayo 7:11 "Basi ikiwa ninyi mwlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je! sizaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?".
Je kwa namna gani mahitaji yetu ya timizwa? Imeandikwa, Mathayo 7:7-8 "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona bisheni nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila aombaye hupokea naye atafutaye ataona, naye abishaye atafunguliwa."
Jambo lamuhimu kuomba ni hekima. Imeandikwa, Yakobo 1:5-8 "Lakini mtu kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapeaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote, maana mwenye shaka nikama wimbi bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani yakuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wania mbili husita-sita katika njia zake zote."
Kwanijia gani Mungu hatayasikia maombi yetu? Imeandikwa, Zaburi 66:18-19 "Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Hakika Mungu amenisikia. Amesikiliza sauti ya maombi yangu."
Je Mungu hukataa kusikiliza maombi? Imeandikwa, Mithali 28:9 "Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria hata sala yake ni chukizo."
Tuombe kwa jina gani? Imeandikwa, Yohana 14:13-14 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukunzwe ndani ya mwana mkiomba neno lo lote kwa jina langu nitalifanya[Yesu]."
Usisahau kumshukuru Mungu kwa kuyajibu maombi yako. Imeandikwa, Wafilipi 4:6 "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru hajazenu zijulikane na Mungu."
Tuombe mara ngapi kwa siku? Imeandikwa, Waefeso 6:18 "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho mkikesha kwa jambo hili na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote."
1Wathesalonike 5:17 "Ombeni bila kukoma."
Wakati mwingine Mungu hujibu maombi yetu kabla hatuja yaomba. Imeandikwa, Isaya 65:24 "Naitakuwa ya kwamba kabla hawajaomba, nitajibu na wakiwa katika kunena, nitasikia,."
Wakati mwingine Mungu hukata kuyajibu maombi yetu. Imeandikwa, 2 Wakorintho 12:8-9 "Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kinitoke, naye akaniambia neema yangu ya kutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu."
Wakati mwingine Mungu huwema ngoja kidogo. Imeandikwa, Zaburi 37:7 "Ukae kimya mbele za Bwana nawe ungojee kwa saburi usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake wala mtu afanyaye hila."
Munug mimwenye uwezo hakuna kilicho gumu kwake. Imeandikwa, Waefeso 3:20 "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu."
Je Mungu ameahidi kuyajibu maombi yetu kadiri gani?. Imeandikwa, Wafilipi 4:19 "Na Mungu wangu atawajazieni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Yesu Kristo."
Je nitajuaje ninachotaka kuomba?. Imeandikwa, Warumi 8:26-27 "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu."
Katika hali gani Kristo amesema tutapata majibu ya maombi yetu?. Imeandikwa, Marko 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia yo yote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu."