Ni wakati gani masahihisho huwa baraka? Imeandikwa katika Wagalatia 2:11 "Lakini Kefa alipokuja Antiokia nalishindana naye uso kwa uso kwa sababu alistahili hukumu."
Masahihisho hufaa wakati yanapofanywa kwa upendo. Imeandikwa katika 1Wakorintho 4:14 "Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao."
masahihisho ni ya maana ikiwa mtu anataka kukua kiroho. Imeandikwa katika Waebrania 12:7 "Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?"
Maandiko ni chemichemi ya marekebisho ya maisha ya watu. Imeandikwa katika 2 Timotheo 3:16-17 "Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa kuonya watu makosa yao na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."