Omba usiwe na mapatano na majaribu Imeandikwa Mathayo 26:41 "Kesheni mkiomba msijemkaingia majaribuni; roho I rathi lakini mwili uthaifu."
Usijaribu hata kidogo kuanza kufuata njia ya uovu. Imo katika Biblia, Mithali 4:14-15 "Usiingie katika njia ya waovu, wala usitembee katika njia ya wabaya. Jiepushe nayo usiipite karibu nayo, igeukie mbali ukaende zako."
Usiwaache wenye dhambi wakuvute. Imeandikwa katika Mithali 1:10 "Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali."
Mtu mkamilifu hakubaliani na wenye dhambi. Imeandikwa katika Isaya 33:15-16 "Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akungu'utaye mikono yake ipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu afumbaye macho yake asitazame uovu huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma."
Si lazima upatane na uovu. Imeandikwa katika 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikupata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila mungu ni mwaminifu ambaye hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea ili mweze kustahimili."
Usimpe shetani nafasi. Imeandikwa katika Waefeso 4:27 "Wala msimpe ibilisi nafasi."
Hakuna mapatano juu ya dhambi, uwe upande wa Mungu au wa shetani imeandikwa Mathayo 12:30 "Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiye kusanya nami hutapanya."