Mwili

Mungu ndiye muumbaji wa miili yetu. Imeandikwa katika Zaburi 139:14 "Nita kushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana. Lazima tuilinde miili yetu kama kafara takatifu imeandikwa katika Warumi 12:1 "Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenyu yenye maana."

Kiroho mwili wako ni mali na hekalu la Mungu. Imeandikwa katika 1Wakoritho 6:19-20 "Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho mtakatifu aliye ndani yenu mliye pewa na Mungu? wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa mtukuzeni Mungu katika miili yenu."

Mwili wako ni wa mke au mume wako. Imo katika Biblia, 1Wakoritho 7:2-4 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe Mume na ampe mkewe haki yake na vivyo hivyo na mke ampe mumewe haki yake mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe."

Baada ya kufa tutafufuliwa. Imo katika Biblia, 1Wakoritho 15:42 "Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika

Mwili ni mfano wa kanisa. Imeandikwa katika Warumi 12:4-5 "Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi wala viungo vyote havitendi kazi moja, vivyo hivyo sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo na viungo kila mmoja kwa mwenzake."