Matokeo ya dhambi ni kifo. Imeandikwa katika Warumi 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Watu huvuna matendo yao. Imeandikwa katika Wagalatia 6:7-8 "Msidanganyike mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu ndicho atakachovuna maana yeye apandaye kwa mwili wake katika mwili wake atavuna uharibifu bali yeye apandaye kwa Roho kwa Roho atavuna uzima wa milele."
Utahudumiwa kiasi cha jinsi unavyowahudumia wengine. Imeandikwa katika Mathayo 7:1-2 "Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakachopimiwa."