Je! mke mwema apaswa kuwa vipi?. Imeandikwa Mithali 31:10-29, "Mke mwema ni nani awezaje kumwona maana kima chake chapita kima cha marijani, moyo wa mume humwamini wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala simabaya, siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. Afanana na merikabu za biashara; huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka kabla haujaisha usiku; huwapa watu wa nyumbani mwake chakula na wajekazi wao sehemu zao. Huanagalia shamba akalinunua; kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viuno kama mshipi; hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidha yake ina faida; taa yake haizimiki usiku hutia mikono yake katika kusokota na mikono yake kuishika pia Huwakunjulia maskini mikono yake Naam huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hwahofu theluji watu wa nyumbani mwake maana watu wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo mavazi yake ni kitani safi na urujuani mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza..."
Je wake wapaswa kuhusiana vipi na bwana zao? Imeandikwa, Waefeso 5:22-24 "Enyi wake watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama Kristo ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo." 1Petro 3:1-5 yasema "Kadhalika ninyi wake watiini waume zenu; kusudi ikiwa wako wasio liamini neno wavutwe kwa mwenendo wa wake zao pasipo lile neno wakiutazama mwenendo wenu safi, na wahofu kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje yani kusuka nywele na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyo haribika yani roho ya upole na utulivu, iliyo ya dhamani kuu mbele za Mungu maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani walio mtumaini Mungu na kuwatii waume zao."
Je inamaana kuwa weke wawe ndio kufanya kazi zote? la ndoa inhitaji kushukuliana na kunyenyekeana. Imeandikwa, Wefeso5:21 "Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo."