Home / Masomo ya Biblia / Majaribu

Majaribu

Unapojaribiwa kumbia upande mwingine. Imeandikwa, 2Timotheo 2:22 "Lakini zikimbie tamaa za ujanani ukafuate haki na imani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi."

Omba upate nguvu za kushinda majaribu. imeandikwa, Marko 14:38 "Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni rorho I radhi bali mwili ni dhaifu."

Tumia neno la Mungu kuzuia majaribu. Imeandikwa Mathayo 4:1, 3, 4, "Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani iliajaribiwe na ibilisi majaribu akamjia akamwambia ukiwa ndiwe mwana wa Mungu amuru kwamab mawe haya yawe miketa, naye akamjibu akasema imeandikwa matu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu."

Mungu hataruhusi tujaribiwe zaidi ya uwezo wetu. Imeandikwa, 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo la kawaida ya wanadamu ila Mungu ni mwaminifu ambaye hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea ilimweze kustahimili."

Wale ambao hawata kubali kuaguka katika majaribu wata barikiwa. Imeandikwa, Yakobo 1:12 "Heri mtu astahimiliye majaribu kwa sababu akisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowahidia wampendao."