Home / Masomo ya Biblia / Mabadiliko

Mabadiliko

Kristo anatuhimiza sisi wenye dhambi tufanye mabadiliko. Imeandikwa katika Yohana 8:10-11. "Yesu akajiinua ila asimuone mtu ila yule mwanamke, akamwambia mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je? Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia hakuna BWANA, Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Nenda zako wala usitende dhambi tena."

Mabadiliko ya Mungu ni kamili. Imeandikwa 2 Wakorintho 5:17. "Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya; yakale yamepita tazama! yamekuwa mapya."

Mabadiliko ya ndani yapaswa yaonekane nje. Imeandikwa katika Mathayo 3:8 " Basi zaeni matunda yapasayo toba."