Ukosoaji waweza kuleta uharibifu. Imeandikwa katika Wagalatia 5:15 "Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana."
Kukosoa wengine mara kwa mara hufunika hitaji la kujikosoa. Imeandikwa katika Mathayo 7:1-5 "Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi, kwa kuwa hukumu hiyo mhukumuyo ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndungu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? au utamwambiaje nduguyo, niache nikitoe kibanzi kilicho jichoni lako na kumbe kuna boriti katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe boriti katika jicho lako wewe mwenyewe ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndungu yako."
Kusamehe ni mwanzo wa kumrekebisha mwenzako. Imeandikwa katika Luka 17:3 "Jilindeni; kama ndugu yako akikosea, mwonye; akitubu msamehe."
Jihadhari na kumlaumu mwingine. Imeandikwa katika Warumi 14:1 "Yeye aliye dhaifu wa imani mkaribisheni wala msimhukumu mawazo yake."
Watoao hupokea. Imeandikwa katika Luka 6:37-38 "Msihukumu, ninyi hamtahukumiwa msilaumu, ninyi hamtalaumiwa; achlieni, ninyi mtaachiliwa. Wapeni watu vitu, ninyi mtapewa kipimo cha kujaa na kishindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika ndicho watu watakacho wapa vifuani mwenu, kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa."
Wakristo watajifunza kutokana na ukosoaji ujengao. Imeandikwa katika Mithali 9:8-9 " Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; mkaripie mwenye hekima naye atakupenda. mwelimishe mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwenye haki naye atazidi kuwa na elimu."
Kuweza kuzuia lawama ni kuwa na mafikara mema. Imeandikwa 1Petro 3:16 "Ninyi mwe na dhamira njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo."