Kwa nini kusikiliza ni yambo la muhimu katiaka maisha ya kiroho? Kumsikiliza Mungu ni hatua moja ya kumheshimu. Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 5:1 "Msa akawaita Israeli wote akawaambia enyi Israeli sikizeni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia na kuzitenda."
Kumsikiliza Mungu akinena twapaswa kuwa kimia na kusikiliza. Imeandikwa 1Wafalme 19:12-13 "Na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto lakini Bwana hakuwamo katika moto ule na baada ya moto sauti ndogo ya utulivi. Ikawa eliya alipoisikia alijifunika uso wake katika mavazi yake akatoka akasimama mlangoni mwa pango. Natazama sauti ikamjia kusema unafanya nini hapa eliya?."
Kusikiliza maboa ya kiroho ya fanya tuelimike kutoka kwa watu wengine. Imeandikwa Yakobo 1:19-20 "Hayo mnayajua ndungu zangu wapenzi basi kila mtu awe mwepesi wa kusikia bali si mwepesi wa kusema wala kukasirika, kwa maana hasira ya mwandamu haiitendi haki ya Mungu."