Kama vile nyakati huleta vyakula vizuri vivo hivyo nasi wakristo twapaswa kuleta halinjema katika ulimwengu. Imeandikwa, Mathayo 5:13-14 "Ninyi chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa ikeharibika itatiwa nini hata I kolee? haifai tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu ninyi ni nuru ya ulimwengu mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima."
Yesu aliwaambia watu yakuwa ukubwa huja kwa kuwa mtumishi. Imeandikwa, Mathayo 23:11-12 "Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu na ye yote atakayejikweza atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili atakwezwa."
Yesu alituonya kutofwata jamii. Imeandikwa, 1Yohana 2:15-17 "Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake maana kila kilicho duniani yaani, tama ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima havitokani na Baba bali vyatokana na dunia na dunia inapita pamoja na tama zake bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele."