Mungu ameahidi kutufariji. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:3-4 "Na ahimidiwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijie katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu."